Home Kimataifa Serikali yaweka tarehe mpya ya likizo fupi kwa shule

Serikali yaweka tarehe mpya ya likizo fupi kwa shule

0
kra

Wizara ya Elimu imetangaza tarehe mpya ya likizo fupi kwa shule za msingi na upili katika muhula wa pili ili kufidia muda uliopotezwa baada ya changamoto za mafuriko nchini.

Kwenye mabadiliko hayo yaliyotolewa na katibu wa kudumu katika Wizara ya Elimu Dkt. Belio Kipsang Jumatano, wanafunzi wataenda kwa likizo fupi wa muhula wa pili kuanzia Juni 26 na kurejea shuleni Juni 28, 2024.

kra

Kulingana na ratiba ya hapo awali, likizo fupi ya muhula wa pili ulitarajiwa kuanza mnamo Juni 20 hadi 23, 2024.

“Mabadiliko yanaweza kuhitaji marekebisho kwenye shughuli zilizopangwa na ratiba. Kwa hivyo umeelekezwa kuwasilisha maudhui ya waraka huu kwa Walimu Wakuu na Wakuu wote wa shule zilizo chini ya mamlaka yako,” akasema Dkt Kipsang, kwenye waraka kwa Wakurugenzi wote wa Elimu wa Kaunti.

Ufunguzi wa shule katika muhula wa pili uliratibiwa mnamo Aprili 29.

Hata hivyo, wizara ya Elimu ikaahirisha hadi Mei 6 kutokana na mafuriko yaliyoshuhudiwa nchini. Baadaye serikali ikaahirisha tena hadi muda usiojulikana.

Mnamo Mei 8, Rais William Ruto akatangaza shule kufunguliwa Jumatatu, Mei 13, idara ya utabiri wa hali ya hewa ilipotangaza kupungua kwa mvua.

Alphas Lagat
+ posts