Home Kimataifa Serikali yaunda kamati ya kutathmini mfumo wa kufadhili elimu

Serikali yaunda kamati ya kutathmini mfumo wa kufadhili elimu

0
kra

Serikali imeonekana kulegeza msimamo na kubuni kamati mbili zitakazotathmini mfumo mpya wa kufadhili elimu ya vyuo vikuu.

Akitangaza hayo Jumapili, Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba amesema kamati hizo mbili zitasikiza maoni ya wanafunzi na kutoa mapendekezo mwafaka kuhusiana na mfumo huo.

kra

Ogamba amewataka wanafunzi kufutilia mbali maandamano  yaliyopangiwa kesho.

Kamati hizo zitaangazia jinsi ya kusuluhisha changamoto zinazokabili mfumo huo wa elimu na pia kutathmini upya mikopo ya masomo inayotolewa.

Haya yamejiri baada ya viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu  kutoa taarifa Jumapili kuhusu azima yao ya kuandamana kesho kote nchini, kupinga mfumo huo wa kufadhili wanafunzi.

Wanafunzi wamekuwa wakilalama kuhusu kuwekwa kwenye makundi wasiyostahili wakati wa kupokea ufadhili wa masomo, hali iliyochangia wengi wao kushindwa kumudu kugharimia kozi zao.

 

Website | + posts