Home Habari Kuu Mswada wa Fedha 2024: Serikali yadhihirisha ubabe bungeni

Mswada wa Fedha 2024: Serikali yadhihirisha ubabe bungeni

0
Bunge la taifa.
kra

Serikali jana Alhamisi ilitumia ubabe wa wabunge wengi ilio nao bungeni kupitisha Mswada tata wa Fedha wa mwaka 2024 kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya pili. 

Mswada huo umekumbana na pingamizi kali kutoka kwa Wakenya, na vijana wengi wanaofahamika kama Gen Z wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mbalimbali nchini kuwashinikiza wabunge kuutupilia mbali.

kra

Wabunge wa mrengo wa Azimio walikuwa wameapa kufanya kila wawezalo kuuangusha bungeni.

Hata hivyo, jana Alhamisi, wakati nchi hiyo ilifuatilia vikao vya bunge la taifa vilivyorushwa mubashara katika vyombo vya habari, idadi isiyotosheleza ya wabunge wa Azimio bungeni ilidhihirika.

Jumla ya wabunge 204 wanaoegemea mrengo unaotawala wa Kenya Kwanza waliunga mkono mswada huo wakati wa kupiga kura huku 115 wakiupinga.

Wabunge walipitisha mswada huo licha ya shutuma kali kutoka kwa Wakenya, ikiwemo maelfu ya waandamanaji waliofurika barabarani katika zaidi ya kaunti 10.

Wakenya wengi wanahofia kuwa mswada huo huenda ukaongeza gharama ya maisha ambayo tayari imewaelemea.

Baadhi ya mapendekezo katika mswada huo ni kuongeza ushuru wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kama njia ya kukuza ustawi wa viwanda vya humu nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here