Wizara ya Leba na ulinzi wa jamii imetoa shilingi bilioni 3.2 yakiwia malipo ya mwezi Juni chini ya mpango wa Inua Jamii.
Malipo hayo yanalenga kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum katika jamii wakiwemo yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, wazee, watu wenye ulemavu na wale walio chini ya mpango wa kupokea msaada wa vyakula.
Katibu wa ulinzi wa jamii Joseph Motari, amesema wamesajili watu 570,263 wapya wamesajiliwa katika mpango wa Inua Jamii na kufikisha idadi ya watu 1,607,996 kufikiwa mwisho wa mwezi Juni mwaka huu.
Motari ameongeza kuwa walionufaika watapokea malipo kuanzia Jumatano hii kupitia kwa akaunti za benki.
Mpango huo ulipanuliwa kufuatia agizo la Rais William Ruto mwaka jana aliyetaka idadi ya wanaonufaika kuongezwa hadi kufikia watu milioni 2.5.
Mpango wa Inua Jamii ni mpango wa serikali uliobuniwa ili kutoa msaada wa kifedha kwa makundi mbalimbali ya jamii, kuwasaidia kukidhi mahitaji yao ya kimsingi na kuboresha maisha yao .