Home Habari Kuu Serikali yatoa shilingi bilioni 2 za Inua Jamii

Serikali yatoa shilingi bilioni 2 za Inua Jamii

0

Serikali imetoa shilingi bilioni 2.09, yakiwa malipo kwa waliojisalili kwa mpango wa Inua Jamii na kiwango kingine cha shilingi milioni 6.1 kwa mpango wa lishe bora, afya na elimu, NICHE.

Haya yametangazwa Ijumaa na Katibu wa Maslahi ya Kijamii na Wakongwe Joseph Motari.

Kila Mkenya aliyejisajili kwa mpango wa Inua jamii atapokea malipo ya shilingi 2,000 kuanzia Disemba 4 yakiwa malipo ya mwezi Novemba.

Mpango wa Inua Jamii unawalenga watu wenye mahitaji maalum kwenye jamii kama wakongwe ambao hupokea pesa hizo kutoka serikali kila mwezi ili kujikimu kimaisha.

Website | + posts