Home Habari Kuu Serikali yatangaza kufunguliwa kwa shule kaunti za Nairobi, Kisumu na Mombasa

Serikali yatangaza kufunguliwa kwa shule kaunti za Nairobi, Kisumu na Mombasa

0

Serikali imetanga kurejelewa kwa masomo katika shule zote za msingi na sekondari za kutwa katika kaunti za Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa  Jumatano, Mawaziri Prof. Kithure Kindiki wa Usalama wa Taifa na Ezekiel Machogu wa Elimu, walisema hatua hiyo imeafikiwa baada ya serikali kukadiria hali ya usalama katika kaunti hizo tatu na kudhibitisha kuwa hali ya kawaida ya usalama imerejelewa.

“Baada ya kukadiria hali ilivyo, serikali imeagiza kufunguliwa tena kwa shule zote za msingi na sekondari za kutwa, katika kaunti za Nairobi, Kisumu na Mombasa tarehe 20 mwezi Julai mwaka 2023,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha Mawaziri hao wawili walidokeza kuwa serikali imechukua hatua madhubuti kuhakikisha usalama wa wanafunzi na shule zao kote nchini.

Mnamo siku ya Jumanne, serikali iliagiza kufungwa kwa shule zote za msingi na sekondari katika kaunti hizo tatu, ikidokeza kuwa wahalifu walipanga kuzua vurugu dhidi ya umma wakati wa maandamano.

“Serikali imepokea taarifa za kiusalama za kijasusi kwamba wahalifu wanapanga kuzua vurugu dhidi ya umma na kukabiliana na maafisa wa usalama karibu na shule fulani ndani ya kaunti za Nairobi,Kisumu na Mombasa,” walisema mawaziri Kindiki na Machogu siku ya Jumanne.

Kulingana na serikali hatua ya kufunga shule siku ya Jumatano, ililenga kuhakikisha usalama wa wanafunzi.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here