Home Habari Kuu Serikali yatakiwa kuwachukulia hatua kali wanaosambaza mbolea bandia

Serikali yatakiwa kuwachukulia hatua kali wanaosambaza mbolea bandia

Viongozi hao walisema mbolea hizo bandia zitasambaratisha juhudi za kuhakikisha uzalishaji wa chakula cha kutosha hapa nchini.

0
Mbolea bandia yapatikana katika sehemu tofauti za nchi.

Viongozi wa kanisa na kisiasa katika kaunti ya Embu, wametoa wito kwa Rais William Ruto kuwachukulia hatua kali wanaosambaza mbolea bandia hapa nchini.

Walisema kupatikana kwa mbolea bandia katika ghala za Halmashauri ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao, NCPB ni jambo la kusikitisha, ikizingatiwa kuwa uzalishaji wa chakula cha kutosha ni miongoni mwa ajenda kuu za utawala wa Rais Ruto.

Wakiongozwa na kasisi Nicholas Makau wa kanisa Katoliki eneo bunge la Mbeere Kusini, kaunti ya Embu, viongozi hao walielezea hofu kuwa mbolea hizo bandia zitasambaratisha juhudi za kuhakikisha uzalishaji wa chakula cha kutosha hapa nchini.

Kasisi Makau alisema ni jukumu la serikali kuwalinda wakulima dhidi ya wanabiashara walaghai na usambazaji wa pembejeo ghushi.

Matamshi yake yaliungwa mkono na mwakilishi wadi ya Makima Philip Nzangi, aliyetoa wito wa kukamatwa na kushtakiwa kwa wale wanaohusika katika sakata hiyo.

Website | + posts