Home Biashara Serikali yatakiwa kudhibiti kudorora kwa sarafu ya Kenya

Serikali yatakiwa kudhibiti kudorora kwa sarafu ya Kenya

Katibu mkuu wa COTU alihimiza wizara ya fedha na benki kuu ya Kenya kuchukua hatua za dharura ili kufanikisha mpango huo.

Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli.

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi humu nchini-COTU Francis Atwoli, amehimiza serikali kuweka mikakati ya dharura ili kudhibiti kudorora kwa thamani ya sarafu ya Kenya.

Atwoli alielezea wasiwasi kwamba sarafu ya nchi hii imeendelea kupoteza thamani yake dhidi ya dola katika siku za hivi punde, na hivyo basi kutishia ustawi wa uchumi wa taifa hili.

Katibu mkuu huyo wa COTU alihimiza wizara ya fedha na benki kuu ya Kenya kuchukua hatua za dharura ili kufanikisha mpango huo.

Alikariri kuwa hali hiyo ikiendelea itaongeza gharama ya maisha, hali ambayo itawaathiri pakubwa wakenya wengi.

Atwoli aliongeza kwamba kuzorota kwa sarafu ya Kenya kunaathiri biashara ya kimataifa kwa vile inahujumu biashara ya kimataifa kwani kunatatiza uagizaji wa bidhaa muhimu kutoka ugenini.

Kwa sasa, sarafu ya Kenya imepoteza thamani yake huku dola moja ya Marekani ikibadilishwa kwa shilingi 162 za Kenya.