Home Habari Kuu Serikali yaagiza kutimuliwa kwa afisa mkuu mtendaji wa Athi Water

Serikali yaagiza kutimuliwa kwa afisa mkuu mtendaji wa Athi Water

0

Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei ameagiza bodi ya usimamizi ya shirika la Athi Water, kumsimamisha kazi afisa mkuu mtendaji Michael Thuita ili kutoa fursa kwa uchunguzi kufanyika kuhusu utoaji kandarasi kwa njia isiyofaa kwa ujenzi wa miradi ya maji ya Ruiru II, Karimenu na Kitui Matuu.

Wakati huo huo Koskei aliagiza bodi ya usimamizi ya shirika la Central Rift Valley, kumsimamisha kazi afisa mkuu mtendaji  Samuel Ouma kutoa fursa kwa uchunguzi kufanyiwa kuhusu  ununuzi usiofaa wa vifaa usambazaji maji kwa miradi ya maji ya Bomet, Longisa na Mulot.

Kupitia kwa barua kwa wenyeviti wa bodi hizo, mkuu huyo wa utumishi wa umma alishangaa ni kwanini bado wangali afisini huku uchunguzi ukiendelea.

Kulingana na Koskei hatua ya bodi hizo kuchelewa kuchukua hatua kunahujumu juhudi za serikali za kukabiliana na ufisadi.