Home Kimataifa Serikali ya Morocco kuwajengea nyumba watu elfu 50 walioathiriwa na tetemeko la...

Serikali ya Morocco kuwajengea nyumba watu elfu 50 walioathiriwa na tetemeko la ardhi

Tetemeko hilo la ardhi la ukubwa wa 6 nukta 8 katika vipimo vya richa lilisababisha zaidi ya vifo 3,000 na idadi sawa ya majeruhi huku zaidi ya watu wengine 50,000 na ushei wakiachwa bila makao.

0

Serikali ya Morocco  imetangaza  mpango wa  kuwajengea makazi mapya   familia elfu 50 zilizopoteza makao kutokana na  tetemeko baya zaidi la ardhi  mapema mwezi huu.

Mfalme Mohammed wa sita wa Morocco, alitangaza hayo siku ya Alhamisi baada ya kufanya kikao na maafisa wakuu serikalini katika kasri lake jijini Rabat.

Kulingana na mpango huo ,awamu ya kwanza itashirikisha kujengwa kwa makazi ya watu 50,000, ambao aidha nyumba zao ziliharibika kabisa au zilibomoka kiasi katika mikoa mitano iliyogongwa na tetemeko hilo la ardhi.

Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita akiwa kwenye mkutano

Serikali pia ilitangaza msaada wa Dirhams 30,000 za Morocco sawa na shilingi 430,000 za Kenya kwa kila mwathiriwa na kiwango kingine cha shilingi milioni 2 kwa kila familia ambayo nyumba yao iliharibiwa kabisa na shilingi milioni 1 kwa wale ambao nyumba zao ziliharibiwa kiasi ili kujenga upya nyumba hizo.

Tetemeko hilo la ardhi la ukubwa wa 6 nukta 8 katika vipimo vya richa lilisababisha zaidi ya vifo 3,000 na idadi sawa ya majeruhi huku zaidi ya watu wengine 50,000 na ushei wakiachwa bila makao.

Website | + posts