Home Kimataifa Serikali ya kaunti ya Nakuru yasambaza dawa za milioni 97

Serikali ya kaunti ya Nakuru yasambaza dawa za milioni 97

0
kra

Serikali ya kaunti ya Nakuru imesambaza shehena ya 4 ya dawa na vifaa vya matibabu vya gharama ya shilingi milioni 97 kuambatana na ahadi ya Gavana Susan Kihika ya kuhakikisha uwepo wa dawa na vifaa katika hospitali za eneo hilo kila wakati.

Kliniki, zahanati na hospitali za Level 4 ndizo zitanufaina na shehena hiyo ya nne.

kra

Naibu Gavana David Kones alifichua kwamba walinunua shehena hiyo kutoka kwa shirika la KEMSA, shirika la MEDS na wauzaji wengine wa humu nchinina inalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na kukabiliana na uhaba katika hospitali.

Shehena hiyo inajumuisha dawa muhimu, vifaa vya maabara, vifaa vya matibabu ya meno, mashuka, vifaa vya matibabu ya saratani kati ya vingine.

Wakati wa kuzindua usambazaji wa shehena hiyo katika afisi kuu za serikali ya kaunti ya Nakuru, Kones alielezea kwamba bidhaa za dawa ni za thamani ya shilingi milioni 45,246,030 na vifaa vya matibabu kwenye shehena hiyo ni vya thamani ya shilingi milioni 52,609,747.

Naibu huyo wa Gavana alihakikishia wakazi wa kaunti ya Nakuru kwa serikali ya kaunti inatafuta ushirikiano na wadau kadhaa katika kuimarisha huduma katika vituo vya afya.

Serikali hiyo ya kaunti ya Nakuru alisema inajibidiisha pia kuweka vifaa vya kisasa katika vituo vya afya ili kuimarisha utoaji huduma.

Kones alimwelekeza waziri wa masuala ya afya katika kaunti ya Nakuru ahakikishe usambazaji wa shehena hiyo unafanikishwa na ifikie walengwa.

Website | + posts