Home Vipindi Serikali ya kaunti ya Kiambu kujenga vituo 130 vya ECDE

Serikali ya kaunti ya Kiambu kujenga vituo 130 vya ECDE

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mazingira bora ya masomo kwa wanafunzi katika kaunti hiyo.

0
kra

Serikali ya kaunti ya Kiambu imeanzisha ujenzi wa vituo vya kisasa ya wanafunzi wa elimu ya chekechea, ECDE.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mazingira bora ya masomo kwa wanafunzi katika kaunti hiyo.

kra

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa 40 ya EDCE katika kaunti ya  Kiambu, Gavana Kimani Wamatangi alisema kila kituo kitakuwa na madarasa mawili ya PP1/PP2, afisi, vyoo na uwanja wa kucheza.

Katika juhudi za kuhakikisha shughuli za masomo zinaendeshwa kwa njia shwari, Wamatangi alisema amejitolea kujenga vituo vipya  130 vya ECDE katika awamu ya kwanza, ujenzi ambao utakakamilika kufikia mwezi Disemba mwaka huu.

Gavana huyo aliwaonya wazazi dhidi ya kuingizwa katika siasa za kupotosha zinazozingiria vituo vya  ECDE vilivyoko katika shule za msingi chini ya uangalizi wa walimu wakuu.

Alisema bunge la kaunti ya Kiambu limepitisha mswada kuhusu mpango wa lishe shuleni.

“Vituo Vyote vya umma vya ECDE vinashiriki katika mpango wa lishe shuleni,” alisema Wamatangi.

Website | + posts