Home Kaunti Serikali ya kaunti kuhamisha familia 1,700 zilizoathirika na mafuriko Homa Bay

Serikali ya kaunti kuhamisha familia 1,700 zilizoathirika na mafuriko Homa Bay

0

Serikali ya kaunti ya Homa Bay inapanga kuhamisha familia 1,700 zilizoathirika na mafuriko .

Kulingana na Mkurugenzi wa mazingira na maji katika kaunti hiyo ya Homa Bay Roy Odongo tayari wameanza kuwaondoa wakazi kutoka maeneo yenye mafuriko kama maeneo ya Karachuonyo, Rangwe, Suba Kaskazini, Suba Kusini, Ndhiwa na Homa Bay Town.

Jumla ya watu 4,785 wameathirika kwa mafuriko katika eneo bunge la Karachuonyo ambapo nyumba kadhaa zimesombwa .

Website | + posts