Home Habari Kuu Serikali na mashirika ya kijamii kuelimisha umma kuhusu vitambulisho vipya

Serikali na mashirika ya kijamii kuelimisha umma kuhusu vitambulisho vipya

Aidha Bitok alidokeza kuwa vitambulisho vya kidijitali vitatolewa kwa hiari.

0

Serikali imeshirikiana na mashirika ya kijamii katika kuelimisha umma kuhusu vitambulisho vipya vya kidijitali vilivyopendekezwa.

Hii inafuatia mkutano ulioandaliwa Jijini Nairobi kati ya katibu katika idara ya uhamiaji na huduma kwa wananchi Julius Bitok na wawakilishi wa mashirika ya kijamii, yakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa Amnesty International Irungu Houghton.

“Lengo kuu ni kukubaliana na mashirika ya kijamii na uwezo wao wa kuhakikisha mchakato huo ni jumuishi. Tunataka wakenya wote kutoa maoni yao kuhusu vitambulisho hivyo vipya,” alisema katibu huyo.

Irũngũ alisema mikutano aina hiyo ni muhimu katika kujadili masharti ya kimsingi yanayopaswa kuafikiwa wakati wa utoaji wa vitambulisho vya kidijitali.

Katibu huyo alisema mashirika ya kijamii yana historia nzuri ya usimamizi bora, akiongeza kuwa serikali itayashirikisha kufikia wananchi wengi.

“Tunataka kushirikiana na wadau wote, tumeandaa mikutano mingine na sekta ya kibinafsi pamoja na viongozi wa kidini,” aliongeza katibu huyo.

Aidha Bitok alidokeza kuwa vitambulisho vya kidijitali vitatolewa kwa hiari.

“Ningependa kuwahakikishia wakenya kwamba hakuna atakayeshurutishwa kuchukua vitambulisho hivyo vipya.

Website | + posts