Home Habari Kuu Serikali kuwatenga fedha wakulima wa miraa na muguka asema Ruto

Serikali kuwatenga fedha wakulima wa miraa na muguka asema Ruto

0

Serikali itatenga shilingi milioni 500 kwa wakulima wa Miraa na Mugukaa katika mwaka wa kifedha 2024/2025, kwa ajili ya kuongeza thamani.

Akizungumza katika ikulu baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa kaunti ya Embu na washikadau kuhusu marufuku ya hivi majuzi ya muguka, Rais William Ruto alisema kuwa lengo lake kuongeza tija ya mazao hayo .

Mkutano huo ulifanywa baada ya serikali za kaunti ya Mombasa na Kilifi, kupiga marufuku usafirishaji,usambazaji,uuzaji na matumizi ya muguka kwa jumla.

Magavana wa kaunti za Mombasa na Embu walikuwa wameafikiana kuhusu hitaji la dharura la udhibiti wa miraa na muguka, huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu athari mbaya za Muguka kwa vijana.