Serikali imeweka mikakati ya kuwarejesha kambini wakimbizi 3,054 waliotoroka kutoka kambi ya Kakuma na kuhamia kaunti ndogo ya Ruiru.
Yamkini wakimbizi hao walitoroka kambi hiyo baada ya jamii mbili kufarakana tarehe 20 mwezi uliopita, hali iliyosababisha familia 762 kutoroka.
Kwenye taarifa iliyotolewa na Idara ya Huduma za Wakimbizi, DRS, serikali kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR imezipatanisha jamii hizo zilizokuwa zikizozana na kurejesha hali ya utulivu.
Idara hiyo na UNHCR itafanya uthibitishaji wa wakimbizi hao upya, kabla ya kuwarejesha kambini.