Home Kimataifa Serikali kuwalipia wanafunzi wote bima ya afya

Serikali kuwalipia wanafunzi wote bima ya afya

0
Rais William Ruto katika shule ya msingi ya Kikuyu Township, kaunti ya Kiambu.
kra

Huduma za Afya zitakuwa bila malipo kwa Wakenya wote kuanzia wakati wanapozaliwa hadi wanapotimia umri wa miaka 18, amesema Rais William Ruto.

Kulingana na Rais Ruto, mpango huo utaanza punde tu bima ya afya ya jamii SHIF itakapoanza kutekelezwa katika muda wa miezi mitatu ijayo.

kra

Kulingana na kiongozi huyo wa taifa, bima ya EduAfya iliyokuwa ikiwahudumia wanafunzi wa shule za sekondari, itapanuliwa ili kuwajumuisha wale wa shule za msingi.

Akizungumza leo Ijumaa alipozuru kaunti ya Murang’a kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo bunge ya Mathioya, Kìharù na Gatanga, Rais Ruto alisema,” Tunabadilisha mfumo wa zamani ambapo bima hiyo ya afya iliwahudumia wanafunzi wa shule za sekondari pekee. Sasa serikali itatoa bima ya afya kwa wanafunzi wote hadi watimie umri wa miaka 18,”.

Wakati huo huo Rais Ruto alisema mpango wa Linda Mama utapanuliwa kwa kina mama, kuwawezesha kuhudumiwa katika vituo vya afya mara kumi kabla ya kujifungua na mara kumi baada ya kujifungua.

Website | + posts