Home Habari Kuu Serikali kuwaajiri walimu 2,000 wa TVET

Serikali kuwaajiri walimu 2,000 wa TVET

Rais Ruto alikariri azma ya serikali ya kutoa rasilmali zaidi kwa sekta ya elimu.

0

Serikali imetangaza kwamba itawaajiri wakufunzi 2,000 wa vyuo vya mafunzo ya kiufundi na kikazi (TVET) kuanzia juma lijalo.

Rais William Ruto amesema kuwa kuajiriwa kwa walimu hao kutaongeza idadi ya wakufunzi katika taasisi za TVET na pia kuboresha uwezo wa taasisi hizo wa kusajili vijana ili wapate ujuzi.

Akizungumza leo Jumanne asubuhi baada ya kuzindua chuo cha utoaji mafuzno kwa wakufunzi wa mafunzo ya kiufundi cha Tinderet katika kaunti ya Nandi, Rais Ruto aliwahimiza wanafunzi waliokamilisha shule wajiunge na vyuo vya TVET ambako wataendeleza mafunzo yao hadi kiwango cha chuo kikuu.

Rais alikariri azma ya serikali ya kutoa rasilmali zaidi kwa sekta ya elimu.

Kuzinduliwa kwa chuo hicho cha Tinderet kutafanikisha kusajiliwa kwa wakufunzi zaidi wa TVET ambao watakapofuzu watapelekwa kwenye taasisi za TVET kote nchini.

Website | + posts
PCS
+ posts