Home Kimataifa Serikali kuu kukamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Kakamega

Serikali kuu kukamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Kakamega

0

Serikali kuu imeelezea dhamira yake ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya mafunzo na rufaa ya Kakamega, KT&RH. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Susan Nakhumicha wakati wa ziara yake katika hospitali ya kaunti ndogo ya Butere leo Ijumaa.

Alikuwa ameandamana na Naibu Gavana Ayub Savula na mbunge wa Butere Tindi Mwale wakati wa ziara hiyo iliyofanyika wakati huduma katika hospitali za umma zimelamazwa kufuatia mgomo wa madaktari ambao umeingia wiki yake ya nne.

Ujenzi wa KT&RH ulioanzishwa na Gavana wa zamani Wycliffe Oparanya umekumbwa na changamoto za kifedha ambazo zimesababisha kukwama kwa ujenzi wake.

Awali, serikali kuu ilitakiwa kuchukua usimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo.

Kumekuwa na mafuriko ya ahadi za kukamilishwa kwa ujenzi wa hospitali hiyo ingawa ahadi hizo husalia kuwa siasa tu za kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wakazi wa eneo hilo.

Nakhumicha amesisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa viongozi wa eneo la magharibi ili kusaidia kukamilishwa kwa ujenzi wa hospitali hiyo.

Mipango ya ukamilishaji huo inajumuisha kupata usaidizi wa kifedha kutoka kwa wawekezaji kutoka India.

 

 

 

Website | + posts