Home Biashara Serikali kutumia ushirikiano wa AGOA kupiga jeki biashara

Serikali kutumia ushirikiano wa AGOA kupiga jeki biashara

Mvurya alisema maafisa kutoka nchi hizi mbili watakutana tena mwezi septemba mwaka huu kujadili maswala ambayo hayajaangaziwa.

0
Waziri wa biashara Salim Mvurya.
kra

Serikali imejitolea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati yake na washirika wake wa kimataifa, katika juhudi za kufanikisha fursa za uwekezaji zinazoongezeka.

Waziri wa uwekezaji,biashara na viwanda Salim Mvurya, amesema Kenya na mataifa mengine ya bara hili yatashinikiza kuongezwa muda wa mkataba wa biashara wa AGOA unaotarajiwa kukamilika mwaka 2025.

kra

Mvurya aliyasema hayo Ijumaa katika mkutano wa wanahabari, baada ya kushauriana na maafisa wa serikali ya Marekani kuhusu mkakati wao wa kibiashara. Ujumbe wa Kenya uliongozwa na katibu wa biashara Alfred K’Ombudo.

“Kutokana na ushirikiano huu, serikali ya Kenya imeanzisha mchakato wa uwekezaji ambao majadiliano yake yangali yanaendelea,” alisema Mvurya.

Mvurya alisema maafisa kutoka nchi hizo mbili watakutana tena mwezi septemba mwaka huu kujadili maswala ambayo hayajaangaziwa.

Alisema serikali imejitolea kuhakikisha inashikilia wadhifa wake wa kuwa mshirika mkuu anayependelewa na Marekani Barani Afrika.

“ Mkataba wa AGOA umekuwa wa manufaa sana kwa kufungua fursa kwa wafanyabiashara wa Kenya kuuza nje bidhaa zao,” alidokeza waziri huyo.

Kwa upande wake katibu katika idara ya biashara Alfred K’Ombudo, alisema ushirikiano huo unalenga kuuza nje bidhaa za kilimo, mabadiliko ya tabia nchi na kuimarisha mazingira ya uwekezaji.

Website | + posts