Home Biashara Serikali kupunguza bajeti kwa shilingi bilioni 500

Serikali kupunguza bajeti kwa shilingi bilioni 500

0

Serikali inapania kupunguza kiwango cha bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa shilingi bilioni 530 katika mojawapo wa juhudi za kupunguza kiwango cha matumizi ya pesa za serikali.

Rais William Ruto amedokeza kuwa analenga kuwasilisha bungeni bajeti ya shilingi trilioni 4.2 hadi trilioni 3.7.

Bajeti ya Kenya imekuwa ikiongezeka kila mwaka kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na ongezeko la idadi ya watu.

Katika bajeti ya sasa ya mwaka 2023/2024, matumizi ya kuradidi yaliongegezeka kwa asilimia 4.4, ikiwa shilingi trilioni 1.6 kutoka kwa bajeti ya mwaka 2022/2023 matumizi hayo yalipokuwa shilingi trilioni 1.5.

Website | + posts