Serikali imetangaza kununua mahindi kutoka kwa wakulima kwa bei ya shilingi 4,000 kwa kila gunia la kilo 90.
Waziri wa Kilimo Mithika Linturi alitangaza kuwa serikali itaanza kununua mahindi kutoka kwa wakulima msimu huu wa mavuno kupitia kwa Halmashauri ya Nafaka na Mazao, NCPB.
Serikali imepanga kununua magunia milioni moja ya mahindi kutoka kwa wakulima kwa gharama ya shilingi bilioni 4.
Hata hivyo, baadhi ya wakulima wanahisi kuwa bei hiyo ni ya chini ikilinganishwa na gharama walizotumia kwa kilimo.
Maoni hayo yanaungwa mkono na Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei anayependekeza bei ya zaid ya shilingi 6,000 kwa kila gunia moja la mahindi.