Home Kimataifa Serikali kumpigia debe Raila Odinga anayesaka uenyekiti wa tume ya AU

Serikali kumpigia debe Raila Odinga anayesaka uenyekiti wa tume ya AU

0
kra

Serikali hivi karibuni itaanzisha kampeni kabambe ya kumpigia debe kiongozi wa upinzani Raila Odinga anayewania wadhifa wa mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika.

Waziri aliye na mamlaka makuu Musalia Mudavadi anasema kwamba Kenya ina imani kwamba kupitia uwaniaji wa Odinga, Afrika Mashariki hatimaye itanyakua wadhifa huo wa kutamanika.

kra

Musalia ambaye pia ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika kaunti ya Lamu ambapo alifafanua kwamba serikali iko makini kushawishi viongozi wa nchi za Afrika kuunga mkono Raila.

Wakati huo huo kiongozi wa walio wengi katika bunge la taifa Opiyo Wandayi ametoa wito kwa wanasiasa kusita kutoa matamshi yanayoweza kuhujumu azma hiyo ya Raila Odinga ya kuwa mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika.

Kulingana naye, mchakato mzima wa kutafuta kuwa mwenyekiti wa tume hiyo ya muungano wa Afrika, unahitaji ushawishi mkubwa wa kidiplomasia barani humu na katika ngazi za kimataifa, na kwamba swala hilo linafaa kuachiwa wataalamu.

Akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa maabara ya shule ya sekondari ya St. Augustine Tingare, kata ya Uholo kaskazini, kaunti ya Siaya, Wandayi alishauri wanasiasa kukoma kuzungumzia suala hilo hadi mwelekeo utakapoafikiwa.

Mbunge huyo wa Ugunja, alisema waziri mkuu wa zamani Raila Odinga au marais 54 wa mataifa ya bara Afrika ndio pekee wanaweza kutoa matamshi kuhusu suala hilo.