Home Biashara Serikali kukopa shilingi Bilioni 333 kuziba nakisi ya bajeti

Serikali kukopa shilingi Bilioni 333 kuziba nakisi ya bajeti

0
kra

Waziri wa fedha na mipango ya uchumi  Prof. Njunguna Ndung’u, Leo Alhamisi amewasilisha makadirio ya matumizu ya fedha za serikali mwaka 2024/2025 ya shilingi Trilioni 3.99. 

Aidha Kulingana na Waziri wa fedha bajeti hiyo Ina nakisi ya shilingi Bilioni 500, hatua ambayo itailazimu serikali kukopa shilingi Bilioni 333.8.

kra

Waziri huyo alisema kuwa serikali itakusanya shilingi trilioni 3.354 kupitia utozaji ushuru, ambapo shilingi trilioni 2.913 zimekadiriwa kutokana na mapato ya kawaida huku shilingi bilioni 441 zikiongezwa kutokana na misaada ya wahisani na mashirika.

Waziri alisema Kenya imeonyesha uthabiti wa uchumi wake katika robo tatu ya kwanza ya mwaka 2023, kiwango ambacho ni wastani, kimataifa na kikanda.

Serikali imekadiria uchumi kukua kwa asilimia 5.5 katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 kufuatia hatua zinazoendelezwa chini ya Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi ya kuwezesha na kuinua wakenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here