Home Taifa Serikali kukagua shule za mabweni za umma na za kibinafsi kote nchini

Serikali kukagua shule za mabweni za umma na za kibinafsi kote nchini

0
Waziri wa elimu Julius Ogamba.
kra

Serikali itaanza awamu ya kwanza ya kukagua shule za mabweni  za umma na zile za kibinafsi, ili kuhakikisha zinazingatia masharti ya kiusalama yaliyowekwa.

Kulingana na Waziri wa Elimu Julius Ogamba zoezi hilo litaendeshwa na maafisa kutoka sekta mbali mbali za serikali  .

kra

Ogamba aliyasema haya  jana katika ikulu baada ya kufanya mkutano na Rais William Ruto.

Haya yanajiri siku chache baada ya wanafunzi 21 wa shule ya Hillside Endarasha Academy kaunti ya Nyeri, kufariki kwenye mkasa wa moto.

Uchunguzi unaendelea kuhusiana na chanzo cha  moto ulioteketeza bweni la shule hiyo ambapo wanafunzi hao wa shule ya msingi walikuwa wamelala.

Website | + posts