Home Biashara Serikali kuimarisha utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini

Serikali kuimarisha utengenezaji wa bidhaa za ngozi nchini

0
Rais William Ruto.

Serikali inalenga kuimarisha utengenezaji wa viatu hapa nchini, hatua itakayolenga kusitisha uagizaji wa viatu kutoka nchi za nje.

Rais William Ruto amesema kuwa serikali itapiga jeki sekta ndogo ya ngozi na hivyo kuinua biashara nyingi hapa nchini.

Akizungumza leo Jumamosi alipoongoza sherehe ya 61 ya Madaraka katika kaunti ya Bungoma, alisema taifa hili litaanza kutengeneza bidhaa kamili za ngozi zinazokubaliwa na zenye ushindani katika masoko ya kimataifa.

Rais alisema serikali inanuia kuongeza mapato kutoka kwa bidhaa za ngozi kutoka shilingi bilioni 15 hadi shilingi bilioni 120 kila mwaka, na kuongeza nafasi za ajira kutoka 17,000 to 100,000.

“Tunalenga kuongeza utengenezaji wa viatu kutoka idadi ya sasa ya viatu milioni nane hadi viatu milioni 36 za thamni ya shilingi bilioni 72 kufikia mwaka 2027,” alisema Rais Ruto.

Rais alisema Kenya inaimarisha uwezo wa kutoa mali ghafi ya ubora wa hali ya juu pamoja na uzalishaji wa bidhaa za ngozi kama vile viatu, mifuko na mishipi.

Kiongozi wa taifa alisema sekta ya kilimo huchangia moja kwa moja asilimia 25 kwa pato jumla la taifa, huku ikitoa asilimia 40 ya nafasi za ajira nchini.

Website | + posts