Home Habari Kuu Serikali kuimarisha usalama katika mipaka ya taifa hili

Serikali kuimarisha usalama katika mipaka ya taifa hili

0
Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Raymond Omollo.

Serikali inajizatiti kuimarisha usalama katika mipaka ya taifa hili, kwa kutambua sehemu za kuingia na kuondoka katika sehemu mbali mbali za nchi.

Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Raymond Omollo, aliyasema hayo siku ya Alhamisi aliongoza ujumbe kutoka kwa kamati ya kudhibiti shughuli za mipakani, kushiriki mkutano wa mashauriano na wakazi wa eneo la  Illeret pamoja na viongozi wa kaunti ya Marsabit wakiongozwa na naibu Gavana  Solomon Gubo, kuzindua eneo la kuingia na kuondoka hapa nchini la Banya Fort kati ya Kenya na Ethiopia.

Katibu huyo aliwahakikishia wakazi hao kwamba kaunti ndogo ya North Horr, itaanza kutoa huduma katika siku 60 zijazo, ili kuleta huduma karibu na wananchi pamoja na kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo.

Website | + posts