Serikali kubuni jopokazi la kubaini pesa zinazopotea kwa siku nchini

Martin Mwanje
1 Min Read

Kuna mipango ya kubuni jopokazi la kubaini ni pesa ngapi za umma ambazo hupotea kwa siku humu nchini. 

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei anasema jopokazi hilo litaanza kufanya kazi hivi karibuni.

Wakati wa utawala wake, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema Kenya hupoteza kima cha shilingi bilioni 2 kwa siku.

Koskei anasema jopokazi hilo litawasilisha ripoti hivi karibuni kubaini ikiwa tathmini ya Rais Mstaafu ni ya kweli ama ikiwa mlipa kodi hupoteza fedha zaidi kuliko hapo.

Serikali itahusisha mshirika wake wa maendeleo katika kufanikisha utafiti huo.

Wakati huohuo, Koskei anasema serikali inapanga kubuni jukwaa litakalotumiwa na raia na mashirika ya kijamii kuripoti visa vya ufisadi.

Mkuu huyo amesisitiza dhamira ya serikali kuhakikisha inaangamiza uovu huo ambao husababisha kupotea kwa mabilioni ya pesa na hivyo kurudisha nyuma kasi ya maendeleo nchini.

Aliyasema hayo leo Alhamisi alipofanya kikao cha mashauriano na mashirika ya kijamii katika ukumbi wa Bomas.

 

 

Website |  + posts
Share This Article