Home Habari Kuu Serikali kuboresha maabara ya uchunguzi wa kifua kikuu

Serikali kuboresha maabara ya uchunguzi wa kifua kikuu

Muthoni alielezea kujitolea kwa wizara yake kuharakisha shughuli hiyo ya ukarabati, kwa lengo la kuimarisha usalama wa wafanyikazi na utoaji huduma bora za afya kwa wakenya.

0

Wizara ya Afya pamoja na washirika wa kimaendeleo inatekeleza mipango ya kuboresha maabara ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu.

Mradi huo unalenga kubadilisha maabara hayo kuwa ya kiwango cha kitaifa (BSL-3), ili kuhakikisha ubora wa hali ya juu.

Katibu katika Idara ya Afya ya Umma Mary Muthoni, alikutana na jopokazi linalotekeleza ukarabati huo jana Jumatatu ili kutathmini mapendekezo yaliyopo.

Jopo hilo lilipendekeza kuwekwa kwa mifumo muhimu kuafikia viwango vya Shirika la Afya Duniani, WHO.

Muthoni alielezea kujitolea kwa wizara yake kuharakisha shughuli hiyo ya ukarabati, kwa lengo la kuimarisha usalama wa wafanyakazi na utoaji huduma bora za afya kwa Wakenya.

Shughuli zinazotekelezwa za kuboresha maabara hayo ni pamoja na zile za ukarabati wa mfumo wa umeme, miundombinu, kiufundi na ubora wa miongozo.

Website | + posts