Home Kimataifa Serikali kuanzisha awamu mpya ya kuwasajili wakulima

Serikali kuanzisha awamu mpya ya kuwasajili wakulima

Serikali ilipunguza bei ya mbolea ya kilo 50 kutoka shilingi 7,000 hadi 2,500.

0
kra

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema serikali itanzisha awamu mpya ya kuwasajili wakulima, huku ikiendelea kusambaza mbolea iliyopunguzwa bei.

Akizungumza Jumamosi katika eneo la North Rift, naibu huyo wa Rais alisema usajili huo unalenga wakulima ambao hawakuwa wamesajiliwa hapo awali.

kra

“Tunaanza awamu ya pili ya usajili wa wakulima watakaopata mbolea. Watu wanapaswa kukoma kushiriki maandamano badala yake wasajiliwe ili wapate mbolea ya gharama nafuu,” alisema naibu wa Rais.

Aliyasema hayo alipozindua usambazaji wa mbolea ya bei nafuu katika ghala la halmashauri ya nafaka na mazao katika eneo bunge la Aldai.

Alielezea ufanishi mkubwa katika mpango wa usambazaji wa mbole hiyo ya bei nafuu, akiongeza kuwa wakuliwa walionufaika na awamu ya kwanza ya mpango huo, wanatarajia mavuno ya kumezewa mate mwaka huu.

“Mavuno ya mwaka huu ya mahindi yataongezeka. Kwa sasa tunatafuta vifaa vya kutosha vya kukausha mahindi ili wakulima wavipate kwa urahisi. Serikali na wakulima watagawana gharama ya kukausha mahindi,” alidokeza Gchagua.

Aidha Gachagua alisema Rais William Ruto ameziagiza hazina kuu na halmashauri ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB kutenga fedha za kutosha za ununuzi wa mahindi, huku akiahidi malipo hayatachelewa.

“Bei itakuwa bora zaidi na malipo yatafanywa ndani ya saa 48,” aliongeza Gachagua.

Serikali ilipunguza bei ya mbolea ya kilo 50 kutoka shilingi 7,000 hadi 2,500.

Website | + posts