Serikali inatarajia kuanza mazungumzo na vyama vya walimu kuhusu mishahara mipya katika juhudi za kuzuia mgomo wa wiki ijayo.
Mgomo ambao umeitishwa na vyama vya walimu vya KUPPET na KNUT unatishia kuvuruga muhula wa tatu, wakati shule zitakapofunguliwa juma lijalo.
KUPPET na KNUT vimeapa kugoma endapo serikali haitatoa shiingi bilioni 13.3 zinazohitajika kutekeleza kikamilifu nyongeza ya mshahara katika makubaliano ya CBA ya mwaka 2021/2025.
Miungano hiyo pia inaitaka Tume ya Kuwaajiri Walimu, TSC kuanza mazungumzo mapya ya nyongeza ya mishahara ya mwaka 2026/20230 na kupandishwa vyeo kwa walimu 130,000 waliopita usaili.
Mgomo wa walimu muhula mpya wa tatu kuanzia wiki ijayo, huenda ukaathiri vibaya mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE kuanzia mwezi Oktoba.