Home Habari Kuu Serikali kuajiri wakufunzi 2,000 wa vyuo vya TVET

Serikali kuajiri wakufunzi 2,000 wa vyuo vya TVET

0

Rais William Ruto ametangaza kuajiriwa kwa wakufunzi 2,000 wa vyuo vya kiufundi TVET kote nchini.

Akihutubu wakati wa sherehe za 60 za siku kuu ya Mashujaa,  Rais alisema kuwa hatua hiyo italenga kuongeza uwezo wa vyuo hivyo vya kiufundi kuwafikia wanafunzi wengi wanaohitaji mafunzo ya ujuzi.

Hii inatokana na ongezeko la vyuo vya TVET nchini hadi 3,200 kutoka 90  miaka tisa iliyopita.

Rais alisema awali serikali ilibuni mfumo mpya wa kufadhili elimu ya juu na taasisi za kiufundi, kuwawezesha wanafunzi kutoka familia masikini kupata elimu bila malipo.

“Ufadhili huo unajumuisha mikopo, udhamini wa masomo, na mpango wa serikali wa kuwalipia karo almaarufu bursary,” alisema Rais Ruto.

Aidha kiongozi wa nchi alisema serikali imeongeza ufadhili wa kila mwanafunzi kwa asilimia 40.

Website | + posts