Home Habari Kuu Serikali itashughulikia changamoto katika sekta ya afya, asema Rais Ruto

Serikali itashughulikia changamoto katika sekta ya afya, asema Rais Ruto

0
Rais William Ruto na katibu mkuu wa chama cha KMPDU, Davji Atella.

Serikali itashughulikia changamoto za mara kwa mara zinazowakabili wahudumu wa afya,na ambazo hudumaza juhudi za kuafikiwa kwa huduma za afya kwa wote, hayo ni kwa mujibu wa Rais William Ruto.

Rais alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika sekta ya afya, vikiwemo vyama vya wahudumu wa afya, kwa lengo la kuhakikisha suluhu la kudumu linapatikana kwa changamoto hizo.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo leo Jumamosi, baada ya kushiriki mazungumzo na uongozi wa chama cha madaktari na wataalam wa meno KMPDU, kikiongozwa na katibu wake mkuu Davji Atellah, katika ikulu ya Nairobi.

Kwa upande wake, chama hicho kilielezea kujitolea kwake kuunga mkono ajenda ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wote na kuazishwa kwa bima ya afya ya kijamii NSHI kwa wakenya wote.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, waziri wa afya Susan Nakhumicha na katibu katika idara ya afya ya umma  Mary Muthoni.

Website | + posts