Home Habari Kuu Serikali kuchelewesha ufunguzi wa mpaka wa Kenya na Somalia

Serikali kuchelewesha ufunguzi wa mpaka wa Kenya na Somalia

0

Serikali itachelewesha mipango ya kufungua vituo vya mpakani kati ya Kenya na Somalia kutokana na matishio ya kiusalama.

Akiongea katika kambi ya wakimbizi ya Daadab, Waziri  wa Usalama wa Taifa Kithure Kindiki, alisema  madhumuni ya hatua hiyo ni  kuipa serikali muda wa kutosha, kushughulikia kikamilifu ongezeko la hivi karubini la visa vya mashambulizi ya magaidi na uhalifu wa mpakani.

Wakati huo huo, Kindiki alitangaza mabadiliko ya sera ya usimamizi wa maswala ya wakimbizi, akisema sasa litakuwa jukumu la serikali ya Kenya kusimamia na kuhifadhi data ya wakimbizi wote walioko humu nchini.

Alisema serikali ya Kenya haitalegeza msimamo wake kuhusiana na utekelezaji wake wa sheria ya mwaka 2022 kuwahusu wakimbizi na pia wajibu wake kama nchi mwanachama wa  mikataba ya kimataifa.

Kindiki alisema serikali itawalinda na kuwasaidia wakimbizi wanaotii sheria na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha katika uhalifu kwa manufaa ya wakimbizi na jamii zinazoishi karibu na kambi za wakimbizi.

“Asilimia 99.99% ya wakimbizi, wanatii sheria na tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia. Haha hivyo wengine ni wahalifu na hawatakubaliwa kuhujumu usalama wa taifa,” alisema Waziri Kindiki.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here