Home Kimataifa Serikali inalenga kupanda miti milioni 100 siku ya Jumatatu

Serikali inalenga kupanda miti milioni 100 siku ya Jumatatu

0

Huku taifa hili likijiandaa kwa siku ya upanzi wa miti siku ya Jumatatu tarehe 13, wizara ya mazingira, mabadiliko ya tabia nchi na misitu, imesema serikali inalenga kupanda miti milioni 100 siku hiyo.

Waziri wa mazingira Soipan Tuya, amesema wizara yake inatumia fursa hii ya mvua fupi kupanda miti milioni 500 kote nchini

Kupitia kwa taarifa, Tuya alisema Kuna miche milioni 150 katika taasisi ya utafiti wa misitu, ambayo Iko tayari kwa upanzi.

Ili kuafikia lengo la upanzi wa miti milioni 100 siku ya Jumatatu ijayo, Waziri huyo alidokeza kuwa serikali ya kitaifa imeshirikiana na zile za kaunti na tayari zimetambua maeneo ambako miti hiyo itapandwa.

“Natoa wito kwa kila mmoja kupanda angalau miche miwili siku ya Jumatatu, ili kuafikia lengo letu la kupanda miche milioni 100 siku ya Jumatatu,” alisema Waziri Tuya.

Serikali ilitangaza Jumatatu tarehe 13 kuwa ya kitaifa ya upanzi wa miti, huku kila Waziri aliongoza zoezi hilo kwa angalau kaunti mbili.

Rais William Ruto alisema serikali inalenga kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Website | + posts