Home Biashara Serikali inajizatiti kuhakikisha wafanyakazi wa KQ wanaozuiliwa DRC wanaachiliwa

Serikali inajizatiti kuhakikisha wafanyakazi wa KQ wanaozuiliwa DRC wanaachiliwa

Katibu katika wizara ya mambo ya nje ya Kenya Korir Sing’Oei, kupitia kwa taarifa katika ukursa wa X, amesema mashauriano yanaendelea ili kusuluhisha suala hilo.

0
Ndege ya shirika la Kenya Airways.

Kufuatia kukamatwa na kuzuiliwa kwa wafanyakazi wawili wa shirika la ndege la Kenya Airways, Nairobi imesema kuwa inashauriana na Kinshasa katika juhudi za kuwaachilia huru.

Wafanyakazi hao wawili walikamatwa leo Ijumaa na maafisa wa Kitengo cha ujasusi cha jeshi la nchi hiyo, kwa madai kwamba hawakuna na stakabadhi za forodha za mizigo.

Katibu katika wizara ya mambo ya nje ya Kenya Korir Sing’Oei, kupitia kwa taarifa katika ukursa wa X, amesema mashauriano yanaendelea ili kusuluhisha suala hilo.

Sing’oei alikariri kujitolea kwa serikali kulinda maslahi ya wakenya wanaofanya kazi ngambo.

” Ubalozi wa Kenya nchini DRC, unashughulikia swala hilo. Serikali inathibitisha kujitolea kwake kuwalinda raia wake wanaofanya kazi ughaibuni,” alisema Sing’Oei.

Mnamo Ijumaa asubuhi Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Allan Kilavuka alisema maafisa wa kitengo hicho waliwapokonya wafanyakazi hao wawili rununu zao na kuwazuia,  kuhusiana na stakabadhi za mzigo uliokuwa usafirishwe kwa ndege ya shirika la Kenya Airways.

Shirika hilo la ndege limekashifu kuzuiliwa kwa wafanyakazi hao wawili ikisema hatua hiyo inalenga kuvuruga biashara ya shirika hilo. 

Website | + posts