Home Habari Kuu Serikali imewapa wanawake uwezo wa kujiimarisha, asema Gachagua

Serikali imewapa wanawake uwezo wa kujiimarisha, asema Gachagua

Gachagua aliwasifu wanawake waliochaguliwa katika chama cha UDA na wale walioteuliwa serikali na Rais William Ruto, akisema utendakazi wao ni wa kupigiwa mfano.

0
Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Utawala wa Rais William Ruto umejitolea kuwapa wanawake wa hapa nchi uwezo wa kujiimarisha, hayo ni kwa mujibu wa Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Kulingana na naibu huyo wa Rais, nafasi ya wanawake katika serikali ya Rais Ruto, imebainishwa na imelindwa.

Akizungumza Ijumaa katika ukumbi wa Bomas wakati wa kongamano la wanawake wa chama cha United Democratic Alliance UDA, Gachagua alisema serikali imebuni mazingira bora ya wanawake, kuhakikisha hawakandamizwi.

“Tumehakikisha wanawake hawakandamizwi, na lazima tuunge mkono kikamilifu nafasi yao katika chama katika serikali,” alisema Gachagua.

Aidha Gachagua aliwasifu wanawake waliochaguliwa katika chama cha UDA na wale walioteuliwa serikalini na Rais William Ruto, akisema utendakazi wao ni wa kupigiwa mfano.

“Serikali haitasita kuwawezesha wanawake wengi, ili kutoa mchango zaidi katika maendeleo ya nchi,” aliongeza Gachagua.

Website | + posts