Raia wa kisiwa cha Saint Lucia wamepewa sikukuu ya mapumziko tarehe 27 Septemba mwaka huu, ili kusherehekea ushindi wa bingwa wa Olimpiki katika mita 100 Julien Alfred.
Dhahabu ya Alfred pia ilikuwa medali ya kwanza ya Olimpiki kwa kisiwa hicho kidogo cha Amerika Kaskazini.
Taarifa ya serikali imefafanua kuwa siku kuu hiyo itasherehekewa kwa tamasha la muziki bila malipo.
Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 23 anatarajiwa kurejea nyumbani Septemba 24.
Atakaribishwa na msafara mkubwa wa magari na kuzuru shule moja keshoye na kisha atazindua sanamu yake iliyochongwa kama njia ya kumuenzi.
Alfred pia alinyakua nishani ya fedha ya Olimpiki katika mita 200.