Aliyekuwa Seneta wa kaunti ya Lamu Anuar Loitiptip alifikishwa mahakamani leo Alhamisi na kushtakiwa kwa kupokea shilingi milioni 6 kutokana na kusudio la kuuza gari moja ambalo lilikuwa na stakabadhi ghushi za usajili.
Alikanusha mashtaka yote matatu dhidi yake alipofikishwa mbele ya Hamu Mkuu Gilbert Shikwe.
Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa mnamo Agosti 3, 2022, Loitiptip alighushi cheti cha usajili cha gari hilo na ambacho alidai kilitengenezwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani, NTSA.
Kisha baadaye, Seneta huyo wa zamani alitumia cheti hicho kutaka kumuuzia Samson Malonza gari hilo cha gari ambalo nambari yake ya usajili ni KDA 005C.
Mahakama ilimuagiza kutoa dhamana ya shilingi laki saba pesa taslimu au dhamana ya shilingi milioni moja.