Home Kimataifa Seneta James Murango wa Kirinyaga atajwa mchapa kazi zaidi

Seneta James Murango wa Kirinyaga atajwa mchapa kazi zaidi

Seneta wa Meru Kathuri Murungi, alitajwa wa pili katika utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe mbili na tarehe tano mwezi huu wa Januari, baada ya kupata alama 74.2.

0
Seneta wa Kirinyaga James Murango.
kra

Kampuni ya utafiti ya Politrack Afrika, imemuorodhesha Seneta wa Kirinyaga James Murango kuwa bora zaidi kwa utendakazi, baada ya kupata asilimia 76.7.

Seneta huyo  alijinyakulia alama nyingi kutokana na jinsi anavyotekeleza wajibu wake katika bunge la Seneti, ikiwa ni pamoja na kuchangia pakubwa kubatilisha uuzaji wa kiwanda cha kusaga mchele cha NICE, aliwasilisha hoja zilizolainisha  kahawa, na pia alitetea kusajiliwa kwa chama cha ushirika cha kahawa cha Kirinyaga Slopes.

kra

Seneta wa Meru Kathuri Murungi, alitajwa wa pili katika utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe mbili na tarehe tano mwezi huu wa Januari, baada ya kupata alama 74.2.

Murungi alipigiwa upato kutokana na mchango wake wa kuwasaidia wasiobahatika katika  jamii, kupitia wakfu wa kamashinani. Seneta huyo pia alisifiwa kutokana na bidii yake ya uhakiki wa sheria zinazojadiliwa katika bunge la seneti.

Seneta wa Kitui Enoch Wambua ameorodheshwa wa tatu kwa asilimia 73 kutokana na umahiri katika utekelezaji wa wajibu wake bungeni .

Wanne ni seneta wa Nyandarua John Metho akifwatiwa na Dkt.. Bonny Khalwale wa Kakamega, Karungo Thang’wa wa Kiambu na Moses Kajwang wa HomaBay.

Seneta wa Isiolo Fatuma Dullo ndiye seneta pekee wa kike aliyeorodheshwa katika 20 bora, kwa mujibu wa utafiti huo.

Website | + posts