Home Kimataifa Seneti kusikiliza mashtaka ya kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua

Seneti kusikiliza mashtaka ya kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua

Karani wa bunge la Senate, alithibitisha kupokea ilani kutoka kwa bunge la Senate Jumatano asubuhi.

0
Spika wa bunge la Senate Amason Kingi.
kra

Spika wa bunge la Senetei Amason Kingi ameitisha kikao cha bunge hilo leo Jumatano asubuhi, kusikiliza mashtaka ya kumbandua madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Kupitia kwa gazeti rasmi la serikali, kikao hicho maalum kitaanza saa tatu na nusu asubuhi, kuambatana na sehemu ya 145 (3) (a) ya katiba ya Kenya na sehemu ya 78 (1) ya kanuni za bunge la Seneti.

kra

“Kuambatana na sehemu ya 145 (3) (a) ya katiba ya Kenya  na  sehemu ya 78 (1) ya kanuni za bunge la Senate, naitisha kikao cha bunge la Senate Jumatano Oktoba 9, 2024 saa tatu asubuhi, kusikiliza mashtaka ya kumuondoa afisini Naibu Rais Rigathi Gachagua,” alisema Kingi.

Karani wa bunge la Seneti, alithibitisha kupokea ilani kutoka kwa bunge la Taifa Jumatano asubuhi.

Bunge hilo litaamua iwapo litateua kamati ya wanachama 11 kusikiliza mashtaka hayo, au bunge lote la Seneti kuyasikiliza.

Wakati wa uchunguzi wake, kamati hiyo maalum itamwalika aliyewasilisha mswada huo pamoja na baadhi ya wabunge kutoka bunge la Taifa.

Gachagua pia atakaribishwa au ataruhusiwa kuwakilishwa na mawakili ili kujitetea.

Jumanne usiku, bunge la Taifa lilipiga kura kumuondoa afisini Naibu huyo wa Rais afisini, baada ya wabunge 281 kuunga mkono hoja hiyo na wabunge 44 kuipinga.

Mbunge mmoja hakupiga kura.

Website | + posts