Home Burudani Selena Gomez afichua kwamba hana uwezo wa kupata watoto

Selena Gomez afichua kwamba hana uwezo wa kupata watoto

0
kra

Mwimbaji na mwigizaji Selena Gomez wa umri wa miaka 32 ameshangaza wengi baada ya kukiri kwamba hawezi kupata watoto kutokana na hali yake ya kiafya.

Gomez alisema kwamba amekuwa akiugua ugonjwa wa Lupus ambao ulifanya apandikizwe figo nyingine akiwa na umri wa miaka 24.

kra

Ugonjwa huo huathiri viungo kadhaa vya mwili na ni pale ambapo kinga ya mwili inavamia tishu pamoja viungo. Iwapo ataamua kubeba mimba atakuwa anahatarisha maisha ya mwanawe.

Hata hivyo msanii huyo anatumai kwamba atakuwa mzazi siku moja hata kama ataafikia hilo kwa njia tofauti na wengine. Anasema suala hilo lilimuumiza kimawazo awali lakini ilibidi akubali.

Alisifia mipango kama vile kusaidiwa kubeba mimba au ukipenda “surrogacy” na kulea watoto wasio na wazazi akisema kwamba huenda akafuata mkondo huo.

“Nashukuru sana kwa mipango hiyo. Watu wanatamani sana kuwa wazazi. Mimi ni mmoja wa watu hao.” alisema mwigizaji huyo akiongeza kusema kwamba anatizamia sana safari yake itakavyokuwa.

“Mwisho wa siku sijali. Atakuwa wangu. Atakuwa mtoto wangu.” alisema mwimbaji huyo ambaye yuko katika uhusiano wa kimapenzi na Benny Blanco.

Huku akifafanua kwamba watu wa familia yake hawamlazimishi aolewe na apate watoto Gomez alifichua mipango ya kufunga ndoa na Blanco na kuongeza kwamba halazimishi Blanco kumwoa.

Website | + posts