Home Habari Kuu Sekta ya ubunifu yahimizwa kukumbatia teknolojia kubuni nafasi za ajira

Sekta ya ubunifu yahimizwa kukumbatia teknolojia kubuni nafasi za ajira

0

Serikali imewahimiza wawekezaji katika sekta ya ubunifu, kutumia teknolojia kuzindua nafasi zaidi za ajira ili kukuza uchumi wa taifa hili.

Akiongea wakati wa mkutano wa ubinifu kupitia teknolojia Jijini Nairobi, katibu wa utangazaji na mawasiliano  Prof. Edward Kisiang’ani, alisema serikali inafanya juhudi za kulainisha sekta ya ubunifu nchini.

Katibu huyo alisema serikali itatumia shilingi bilioni 15.1 katika ustawi wa teknolojia ya habari kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji zaidi nchini.

Aliongeza kuwa wanatafuta ufadhili kutoka sekta ya kibinafsi katika juhudi za kuimarisha  sekta ya ubunifu na kustawisha kituo cha teknolojia cha Konza.

“Serikali Iko tayari kuunga mkono sekta ya ubinifu, ili kuwe na nafasi nyingi za ajira. Sekta hiyo Ina fursa nyingi za ajira kwa kuwa serikali haina uwezo wa kumpa kila mtu ajira,” alisema Kisiang’ani.

Katibu huyo alisema wanapania kuwapa wabunifu usaidizi zaidi wa kifedha na kuwawezesha kuhifadhi kazi yao kwa mfumo wa kidijitali.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here