Azima ya Rais wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni Sebb Coe kuwania urais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, IOC imegonga mwamba baada ya sheria mpya za uchaguzi kumfungia nje.
Kulingana na sheria hizo mpya, Coe hatahudumu kwa mihula miwili mwaka ujao katika wadhifa wa urais wa IOC ilivyo kisheria.
Hii ni kwa sababu uanachama wake katika kamati ya IOC unategemea Urais wa Shirikisho la Riadha Duniani ambao atakamilisha kipindi chake mwaka 2027.
Uchaguzi wa IOC utaandaliwa mwezi Machi mwaka ujao, huku Rais atakayechaguliwa akihudumu kwa muda hadi miaka 12.
Ili kuchaguliwa Rais wa IOC, lazima mwaniaji awe mwanachama wa IOC kupitia kuwa Rais wa shirikisho.