Home Michezo Sawe azidisha ubabe wa nusu marathon mjini Riga

Sawe azidisha ubabe wa nusu marathon mjini Riga

0

Sebastien Sawe ameendeleza ubabe wake katika mbio za nusu marathon katika makala ya kwanza ya mbio za dunia za barabarani kwa kushinda  nusu marathon Jumapili mjini Riga,Latvia.

Sawe ametimka mbio hizo kwa dakika 59 sekunde 10 ikiwa rekodi mpya ya mashindano hayo huku fedha ikitwaliwa na Daniel Simiu kwa dakika 59 na sekunde 14, naye Samwel Nyamai akaridhia shaba kwa dakika 59 na sekunde 19.

Kenya ilitwaa ubingwa wa Jumla kwa dhahabu 5,fedha 3 na shaba 4 ikifuatwa na Ethiopia kwa dhahabu 2 fedha 4 na shaba 1 huku Marekani ikimaliza ya tatu kwa dhahabu 1 na shaba 1.

Peres Jepchirchir,Sebastien Sawe na Beatrice Chebet walishinda dhahabu huku dhahabu nyingine mbili zikipatikana kupitia kwa timu za mbio za nusu marathon.

Website | + posts