Home Burudani Sammie na Shawa waomba msamaha

Sammie na Shawa waomba msamaha

0
kra

Wachekeshaji wa Uganda Sammie na Shawa wameomba msamaha hadharani kufuatia igizo lao ambalo lilionekana kuwaghadhabisha wafuasi wa mwanamuziki Bobi Wine.

Wafuasi wa Wine ambaye pia aliwania urais wa Uganda walihisi kwamba igizo hilo halikustahili na lililenga kumkejeli kiongozi huyo.

kra

Awali wawili hao walikataa kuomba msamaha hata baada ya ghadhabu kali dhidi yao lakini sasa wameonekana kunyenyekea.

Kwenye ukurasa wao wa Facebook Sammie na Shawa wrote walisema wameamua kuomba msamaha baada ya kugundua kwamba igizo lao liliumiza hisia za wengi.

“Tafadhali zingatia kwamba nia yetu haikuwa kuumiza yeyote ila kuonyesha tu ubunifu wetu na ucheshi kama wachekeshaji.” ilisema taarifa ya wawili hao.

Waliendelea kushukuru mashabiki wao ambao wanasema wamewaunga mkono na kuwaonyesha mapenzi huku wakiwakosoa.

“Tunajitolea kuwachekesha na kuwapa burudani huku tukizingatia hisia zenu kama watu binafsi na hata makundi.” walisema wachekeshaji hao.

Walielezea kwamba maudhui ya igizo lao yalitokana na mvutano kati ya Wine na maafisa wa polisi ambapo kiongozi huyo wa upinzani aliishia hospitali.

Wine aliumizwa mguu na kopo la gesi ya kutoa machozi ambalo lilifyatuliwa na maafisa wa polisi katika wilaya ya Wakiso.

wakitumbuiza kwenye Comedy Store, wawili hao waliigiza kuhusu tukio hilo wakionyesha kwamba huenda Bobi Wine hakujeruhiwa ila alikuwa anajisingizia tu, hatua ambayo ilikasirisha wafuasi wa kiongozi huyo wa chama cha NUP.

Website | + posts