Home Kaunti Sakaja: Hakutakuwa na ada ya kuingia Uhuru Park

Sakaja: Hakutakuwa na ada ya kuingia Uhuru Park

0

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amesema kwamba hakutakuwa na hitaji la kulipa ada kabla ya kuingia kwenye bustani iliyokarabatiwa ya Uhuru Park jijini Nairobi.

Akizungumza kwenye mahojiano leo, kiongozi huyo wa kaunti ya jiji la Nairobi alisema kwa tamasha inayoendelea katika bustani hiyo kuna malipo ya kuingia lakini ni nafuu.

Kwenye awamu hiyo ya pili ya tamasha ya Nairobi, watoto wanalipa shilingi 50 na watu wazima wanalipa shilingi 100.

Sakaja aliahidi pia kwamba bustani hiyo ya Uhuru na ile ya Central zitazinduliwa rasmi baada ya kufungwa kwa muda mrefu kwa ukarabati.

Huduma ya jiji la Nairobu almaarufu “Nairobi Metropolitan Services” ndiyo ilifunga bustani hizo Februari 2022 kwa lengo la kuziboresha.