Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametangaza kupanua mradi wa lishe shuleni kwa wanafunzi maarufu kama “Dishi La County”, kwa shule za mitaa ya mabanda.
Akizungumza Jumatatu Sakaja amesema hatua hiyo itahakikisha wanafunzi wote wananufaika bila ubaguzi wa shule wanazosoma.
Sakaja alikuwa azungumza Jumamtatu alipozindua awamu ya tatu ya mradi huo ,akiongeza kuwa utasambazwa kwa shule zote za umma katika kaunti ndogo 17 za Nairobi.