Home Habari Kuu Sajenti Nyawira azikwa nyumbani Kirinyaga

Sajenti Nyawira azikwa nyumbani Kirinyaga

0

Sajenti Rose Nyawira aliyefariki kwenye ajali ya ndege ya jeshi wiki iliyopita amezikwa Alhamisi nyumbani kwake kaunti ya Kirinyaga.

Bi Nyawira aliaga dunia pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Francis Ogolla kwenye ajali ya ndege eneo la Kaben kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Wafanyikazi wenza walimtaja Nyawira kuwa mkakamavu na mwenye bidii na aliyependa kazi yake.

Nyawira amezikwa kwa itikadi za kijeshi huku mazishi hayo yakihudhuriwa na maafisa wengine wa jeshi na Gavana wa kaunti ya Kirinyaga ,Anne Waiguru.