Home Habari Kuu Sahau ugavi wa mamlaka, Muthama amuambia Raila

Sahau ugavi wa mamlaka, Muthama amuambia Raila

0

Hapatakuwa na mazungumzo yoyote ya ugavi wa mamlaka kati ya Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. 

Hii ni kwa mujibu wa Seneta wa zamani wa kaunti ya Machakos Johnstone Muthama.

Muthama ambaye pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge, PSC amesema ikiwa majadiliano yoyote yatafanyika kati ya Rais Ruto na Raila, yataangazia tu maslahi ya taifa.

“Majadiliano yataangazia tu masuala yanayowaathiri Wakenya na wala sio maslahi ya mtu binafsi. Hapatakuwa na ugavi wa mamlaka kati ya serikali na upinzani,” Muthama alisema leo Jumatano.

Kauli zake zinawadia wakati ambapo Rais William Ruto ameashiria kuwa yuko radhi kukutana na Raila wakati aupendao.

Kupitia mtandao wake wa Twitter jana Jumanne, Ruto alielezea utayari wake wa kukutana na kiongozi huyo wa Azimio kufuatia matamshi ya Raila kuwa juhudi zake za kutaka kukutana na Rais ili kuangazia masuala yanayoathiri taifa kama vile gharama ya maisha hazijafua dafu.

Awali, Rais Ruto amesisitiza kuwa hapatakuwa na ugavi wa mamlaka kati ya serikali na upinzani.

“Upinzani ni lazima utekeleze wajibu wake wa kuikosoa serikali,” alisema Rais Ruto.

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here